Harry Kane afikisha mechi 100 England.

Mchezaji wa Bayern Munich na nahodha wa timu ya taifa ya England “Three Lion” Harry Kane  amefanikiwa kufikisha mechi 100 ndani ya uzi wa timu ya Taifa lake  baada ya mchezo wa jana septemba 10,2024  uwanja wa Wembley na kufunga magoli mawili (2) dhidi ya Finland kwenye mchezo wa UEFA National League nakufanya taifa hilo kufikisha alama 6 wakiwa nafasi ya pili katika kundi “B”.

Kabla ya mchezo huo Kane alikabidhiwa kofia ya dhahabu ikiwa ni sehemu ya kumpongeza kuwa miongoni mwa wachezaji 10 kufikisha mechi100 wakitumika ndani timu ya taifa la England.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa Uingereza wakipongezana baada ya ushindi wa mchezo mabao 2-0 dhidi ya Finland.

Harry kane ameifungia timu ya taifa magoli 2 nakumfanya kuwa ni mfungaji bora wa muda wote wa England akiwa na magoli 68 kwenye michezo 100 alizo cheza.

Timu ya taifa England yenye ukame wa mafanikio kwenye mashindano UEFA National League inatafuta nafasi ya kushinda mashindano hayo ikiwa hawajawahi kupata taji hilo na imefika hatua ya nusu fainali mara 1,musimu 2018-2019 baada ya kushinda dhid ya uswis kweny mech ya kusaka mshindi wa 3.

Mwandishi;Eunice Jacob.


Post a Comment

0 Comments