Hofu yatanda Mzozo wa Israel na Hezbollah.

Israel imezishambulia ngome za kundi la Hezbollah kusini mwa Lebanon huku Hezbollah kwa upande wao imevishambulia vituo vya kijeshi kaskazini mwa Israel huku watu wa Lebanon wakihama makazi yao.

Mashambulizi hayo yamefanyika usiku wa kuamkia Septemba 24, 2024 huku hali hiyo ikiongeza hofu ya kutokea vita kamili kati ya Israel na Hezbollah wakati Lebanon ikitangaza vifo vya zaidi ya watu 490 wakiwemo watoto 35 vilivyotokea kufuatia mashambulizi ya Israel.

DW imeripoti kuwa mamia ya watu kutoka kusini mwa Lebanon wameonekana kuyahama makazi yao na kutafuta sehemu salama, huku msongamano mkubwa wa magari umeshuhudiwa katika barabara kuu ya kuelekea upande wa kaskazini mwa nchi hiyo.

msururu wa magari uliobeba wakimbizi kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel kwenye barabara kuu inayounganisha mji wa Beirut katika mji wa bandari wa Sidon.

Aidha Waziri wa Lebanon Nasser Yassin anayeshughulikia masuala ya dharura ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, kambi 89 za muda zenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya watu 26,000 zimetengwa kwa ajili ya kuwahudumia maelfu ya watu wanaokimbia makaazi yao kutokana na kile alichokiita ukatili wa Israel.

Katika hatua nyingine kundi Hezbollah, linaloungwa mkono na Iran limeeleza kuwa limevishambulia vituo vya jeshi la Israel kikiwemo kiwanda cha kutengeneza silaha.

Kundi hilo limesema limefanya mashambulizi hayo kwa kutumia roketi aina ya Fadi saa kumi leo alfajiri. Hezbollah imeongeza kuwa, imeushambulia pia uwanja wa ndege wa Megiddo karibu na mji wa Afula kaskazini mwa Israel.

 Wakati huo huoMarekani imetangaza kuongeza idadi  ya wanajeshi wachache huko mashariki ya kati ikiwa ni taadhari ya  mgogoro unaoendelea katika eneo Hilo .

msemaji wa wizara ya ulinzi wa nchi hiyo Meja Jenerali Pat Ryder amesema wamepeleka   wanajeshi wa ziada huko Mashariki ya Kati kufuatia ongezeko kubwa la ghasia kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.

Bw. Ryder hakutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya wanajeshi waliopelekwa huko au kuhusu kile watakachofanya.

Hata hivyo  afisa  mkuu Mmoja ,wa Marekani amesema   kwamba kazi ya  kwanza ya wanajeshi  hao , itakuwa kuwasaidia raia wa Marekani kuondoka katika maeneo  ya hatari   iwapo vita vitazuka katika kanda hiyo yote.

Aidha Afisa huyo amesisitiza kwamba  kwa sasa hali haijafikia kiwango cha kuhitaji usaidizi wa jeshi kuwaondoa raia wa Marekani walioko maeneo hayo .

"Ikibidi kuwaondoa watu, jeshi la Marekani lina wanajeshi waliopelekwa eneo la karibu na watatekeleza kazi hiyo, afisa mwingine ameiambia VOA. Wote waliomba majina yao yasitajwe., 

Mwandishi; Sharifat Shinji

Mhariri; Ramadhan Zaidy

Post a Comment

0 Comments