IOC: yatoa majina saba kuwania Urais


Kamati ya kimataifa ya michezo Olimpiki imetangaza wanachama watakao wania nafasi ya Thomas Bachraia wa Ujerumani ambaye atajiuzulu baada kufikisha miaka 12 akiwa madarakani.

Tarifa hiyo ya IOC imetolewa Septemba 16, 2024 na kamati hiyo huku wakitoa majina saba ya wagombea watakaochuana kuwania nafasi hiyo ya adhimu na bora zaidi katika ulimwengu wa michezo ifikapo Machi 18 hadi 21,2025.

Aidha katika tarifa hiyo ya watu saba watakaowania nafasi hiyo Mwanamke mmoja tu ambaye ni mjumbe wa bodi ya utendaji ya IOC Kirsty Coventry kutoka Zimbabwe, ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuongoza shirika ambalo limekuwa na marais wa kiume pekee katika historia yake ya miaka 130.

Hata hivyo wadau wengi wa soka wameweka mijadala katika mitandao ya kijamii juu ya jina la mwana mama kutoka bara la Afrika huko nchini Zimbabwe kuwa akipata nafasi ataweza kuongoza nafasi hiyo adhimu ulimwenguni.

Hata hivyo hii ni mala ya pili kwa mwanaamke kuingia katika kinyang’anyiro hicho toka afanye hivyo Anita De Frantz, mpiga makasia wa zamani wa Olimpiki kutoka Marekani aligombea na kuondolewa katika duru ya kwanza ya upigaji kura katika uchaguzi wa wagombea watano mwaka 2001, ambae alishindwa na Jacques Rogge.

Mwandishi; Sharfat Shinji 

Post a Comment

0 Comments