ISOC Tanzania yawajengea vijana uwezo wa kimtandao.

                                                                                                                   
Taasisi ya Internet Society Tanzania Chapter(ISOC-TZ) kupitia jukwaa la usimamizi wa mtandao Tanzania 'Internet Governance Forum(TzIGF)' imewataka vijana kujenga uwezo katika masuala ya usimamizi wa mitandao.


Ikiripotiwa na michuzi kuwa mafunzo hayo yamefanyika Septemba 4, Jijini Dar es Salaam, huku  Rais wa ISOC -Tz Nazar Kirama akibainisha kuwa vijana ndio viongozi wa baadae hivyo wanahitaji kujengewa uwezo katika masuala ya usimamizi wa mitandao.

Aidha Kirama amesema kuwa katika upatikanaji wa huduma za mtandao katika baadhi ya maeneo umekuwa wa tabu hivyo vijana wanajukumu kubwa katika kuwashauri  watunga sera juu ya kupata uwiano katika maeneo yote.
Baadhi ya washiriki vijana  katika mafunzo ya usimamizi wa Mtandao yaliyoandaliwa na ISOC Tanzania jijini Dar es Salaam. (Picha:michuzi)

Naye Janeth Kahindi kutoka Taasisi ya TECH and Media Convergency (TMC), amesema mafunzo ni muhimu kwani Dunia ipo katika ulimwengu wa kidigitali hivyo itasaidia vijana kufahamu haki za kimtandao, mipaka pamoja na sheria za kujisimamia kama kijana.

"Ni muhimu zaidi kwa vijana kujifunza masuala haya kwasababu wengi wao wanatumia mtandao katika mambo mbalimbali ikiwemo kutengeneza ajira na pia vijana ni kizazi cha kesho itasaidia kuwa na kizazi salama chenye kujiingizia kipato kupitia mtandao.

Kwa mujibu wa tanzaniaweb ilichapisha mwaka 2021 kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi katika bara Afrika zimekuwa na ongezeke la matumizi ya Internet ikiwa tanznia ilishikanafasi ya 10 katika orodha ya nchi zenye idadi kubwa ya watumiaji wa Internet, Tanzania ikiewa na watumiaji milioni 15.60 tukizidiwa na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ikiwa na idadi ya watumiaji milioni 16.50 huku Nigeria ikishika nafasi ya kwanza ikiwa na watumiaji milioni 109.2.

Mwandishi: Ellukagha kyusa


Post a Comment

0 Comments