Jeshi la Polisi lapiga marufuku Maandamano CHADEMA.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime

Jeshi polisi nchini limepiga marufuku,maadnamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA yaliyokuwa yafanyike jiji  Dar-es-salaam  Septemba 23,2024 yaliyotarajiwa kuhusisha kata na mitaa yote.

Akizumgumza leo Septemba 13,2024 Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime,  amesema Jeshi hilo limetoa katazo kwa yeyote aliyealikwa kufika jijini Dar es Salaam  kutoka mkoa wowote ule kwa ajili ya maandamani hayo asithubutu kufika.

                                          Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime


Mwandishi; Shukurumana Revokatus

Post a Comment

0 Comments