Joto la usaji dirisha dogo ulaya laanza.

Al-Nassr wanamlenga kiungo wa kati wa Manchester City na Croatia Mateo Kovacic, 30, katika dirisha la uhamisho la Januari kwa malipo ya zaidi ya £750,000 kwa wiki.

Mshambuliji wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah, 32, ana nia ya kusaini mkataba mpya ili kuongeza muda wake wa kusalia Anfield.

Liverpool wanapanga kufanya mazungumzo na Salah kuhusu mkataba mpya siku za usoni, The Reds wanatumai kuwa hatma yake itatatuliwa kabla ya dirisha la usajili la Januari. 

Vinginevyo, Liverpool wanatarajia Salah, mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, na kipa wa Brazil Alisson Bekar, 31, wote kuhamia Saudi Arabia msimu ujao. 

Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32, atazingatia ofa za kuondoka Manchester United ikiwa ataambiwa kuwa hana mustakabali Old Trafford. 

Casemiro anaweza kuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo ndani ya siku chache zijazo, Manchester United na Newcastle bado wamechanganyikiwa kuhusu usajili wa kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru huku ofa kutoka kwa Galatasaray ikiwa mezani kwa mchezaji huyo wa zamani wa Juventus. 

Mwandisha: Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments