Kahama yatajwa kinara kwa utoroshaji madini nje ya nchini.

   Waziri wa Madini, Mh: Anthony Mavunde  amewaelekeza maofisa madini wakazi waliopo kwenye mikoa yote nchini kuongeza kasi ya kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini hayo yamejiri baada ya wilaya ya kahama mkoani shinyanga kutajwa kuwa kinara wa utoroshwaji wa madini nje ya nchi hali inayokosesha serikali mapato.

Waziri Mavunde ametoa taarifa hiyo septemba 16,2024 katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maofisa madini wakazi sambamba na maofisa kutoka Wizara ya Madini jijini Tanga na kuataka kuwa na mbinu thabiti ili kuweza kuzuia utoroshaji wa madini.

Aidha mavunde ameongeza kuwa watoroshaji hao wamekuwa wakitumia mashine za kuchakata mpunga ili kuweza kufanikisha zoezi la utoroshaji wa madini.

                   maofisa madini wakazi sambamba na maofisa kutoka Wizara ya Madini

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni, kutoka tume ya madini ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania imepata jumla ya shilingi trilioni 1.877 kutoka kwenye kampuni 44 zilizoshiriki katika sekta ya madini, mafuta, na gesi kwa mwaka wa fedha 2021/22 Kati ya kampuni hizo, 26 ni za madini, 7 ni za gesi asilia na mafuta, na 11 ni kampuni zinazotoa huduma katika sekta hizo.

Sekta ya madini inachangia zaidi ya asilimia 50 ya mauzo ya nje ya nchi, ambapo sehemu kubwa inatokana na dhahabu  kwa mwaka 2022/2023 mchango wa sekta ya madini ni asilimia 9.6." Serikali kupitia sekta ya madini imeweza kukusanya shilingi bilioni 409.66 sawa na asilimia 85.43

Mwandishi; Jenipher Sanga.

Post a Comment

0 Comments