Kashfa ya kingono yamuweka matatani waziri.

Picha; Reprodução da Internet

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amemfuta kazi waziri wa haki za kibinadamu Silvio Almeida, kufuatia madai ya kuwanyanyasa kingono wanawake kadhaa, akiwemo waziri mwenzake.

Taarifa ya ofisi ya rais iliyotolewa septemba 7,2024 imesema kuwa "rais anaona ni jambo lisilofaa kuendelea kumweka waziri ofisini kwa kuzingatia aina ya tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia," ilisema taarifa hiyo.

Kashfa hiyo iliyozua ghadhabu nchini Brazil ni ya kwanza na ya aina yake kumhusisha waziri katikaserikali ya Lula tangu kiongozi huyo mkongwe wa siasa za mrengo wa kushoto aliporejea madarakani mwaka jana.

Ikiripotiwa na DW kuwa tovuti moja ya habari nchini humo ya Metropoles ilisema kuwa shirika la masuala ya wanawake la Me Too Brazil, lilipokea malalamiko dhidi ya waziri huyo kutoka kwa wanawake kadhaa.

Polisi wa shirikisho wamesema kuwa wanayachunguza madai hayo huku tume ya maadili ya rais nayo ikianzisha uchunguzi.

Almeida, mwanasheria na profesa wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 48, amekanusha madai hayo na kudai kuwa yanalenga kumchafua.

Mwandishi; Abel Mahenge


Post a Comment

0 Comments