HATARI! Kasulu vyoo hali tete

Wakazi wa Mji wa Kibiashara wa Kasulu mkoani Kigoma magharibi mwa Tanzania wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kaya nyingi kutokuwa na vyoo bora katika makazi yao.

Hayo yamewekwa bayana na Afisa Afya na usafi wa mazingira katika halmashari ya mji kasulu Msafiri Charles akikiri kuwa  hali ya vyoo katika mji ni mbaya.

Akizungumza Buha News ofisini kwake septemba 24 ameeleza kuwa idara yake imebaini hali hiyo baada ya kuendesha kampeni ya Mtu ni Afya iliyo anzishwa agost 1,2024 na kutembelea katika kata ya Muhunga na mitaa 06 na kubaini kuwa kati ya kaya 103 ni kaya 02 tu zenye choo bora.

Bw. Charles ameongeza kuwa ukosefu wa vyoo bora imekuwa ni changamoto kubwa katika mji huo hivyo inapelekea kuwepo kwa hatari ya kuzuka kwa magonjwa ya milipuko na kuongeza kuwa jamii inahitaji kupata elimu ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Afisa Mtendaji wa mtaa wa Bwanyana Gaston Erasto ameeleza kuwa katika mtaa wake pamekuwa na changamoto ya vyoo kutitia hivyo kupelekea wakazi wa mtaa huo kuogopa kujenga vyoo kwa kuhofia hasara.

   Muonekano wa miundombinu ya choo katika wilaya ya Kasulu mji mtaa wa Bwanyana kata ya muhunga  , Kigoma. (picha na Kasulu TC).

Bw. Erasto anabainisha kuwa wakazi wa Bwanyana wamepewa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa vyoo bora lakini wengi wao wanahofia kuendelea na zoezi la ujenzi wa vyoo bora kutokana na kipindi cha mvua tunachokiendea ambacho kinapelekea vyoo kubomoka amesema Gaston

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo fanya kweli usibaki nyuma lengo likiwa ni kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora na kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Mwandishi; Ellukagha Kyusa

Mhariri; Eunice Jacob





Post a Comment

0 Comments