Kenya kuomboleza siku tatu vifo vya wanafunzi.

   Picha:Ikulu Kenya

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza muda wa siku tatu wa maombolezo ya kitaifa kufuatia mkasa wa moto uliowaka katika bweni la Hillside Endarasha katika kaunti ya Nyeri na kusababisha vifo vya watoto 17.

Katika tangazo lililotolewa siku ya Ijumaa jioni na Rais wa Kenya kwa mujibu wa BBC kuwa siku za maombolezo zitaanza alfajiri Jumatatu, Septemba 9, hadi machweo siku ya Jumatano, Septemba 11, 2024 na kuagiza katika kipindi hiki, bendera za Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki zipeperushwe nusu mlingoti kote nchini.

“Kwa masikitiko makubwa na heshima ya kumbukumbu ya maisha ya watu wasio na hatia waliopoteza maisha na wale waliojeruhiwa katika mkasa huu, ninatoa agizo hili kuelekeza kwamba,Kenya itaadhimisha muda wa siku tatu kwa ajili yamaombolezo kwa Taifa.

Katika kipindi hiki cha maombolezo ya kitaifa, Bendera ya Jamhuri ya Kenya na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) itapeperushwa nusu mlingoti Ikulu, Balozi zote za Kenya, Majengo ya Umma, Viwanja vya Umma , Vituo vyote vya Kijeshi, Meli zote za Wanamaji za Jamhuri ya Kenya, na katika eneo lote la Jamhuri ya Kenya, kuanzia alfajiri ya Jumatatu, tarehe 9 Septemba 2024 hadi machweo ya Jumatano, tarehe 11 Septemba 2024.

Rais alielezea huzuni ya pamoja ya taifa, akitoa salamu zake za rambirambi kwa familia zilizopoteza watoto wao kwa moto na kusema kuwa wamelazimika kuwajibika katika shule zote nchini kunachukuliwa hatua za uangalizi ili kulinda maisha ya wanafunzi juu ya majanga ya moto.

katika ujumbe wake uliochapishwa kwenye mtandao wa X , Rais wa Kenya William Ruto amesema kwamba anaomboleza vifo vya watoto hao na kuitaka polisi pamoja na idara ya zima moto kufanya uchunguzi kamili wa chanzo cha moto huo na watakaopatikana na hatia kufunguliwa mashtaka.

Mwandishi;Ellukagha Kyusa

Post a Comment

0 Comments