Jumla ya miradi kumi yenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni 4 imekaguliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.
Akisoma taarifa ya
miradi hiyo mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amesema kuwa
miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na miradi ya maji, afya, barabara na elimu.
Kwa upande wake mbunge
wa jimbo la Muhambwe Dr. Frolence Samizi amesema kuwa serikali inaendelea
kufanya kazi kubwa ya kuboresha miundo mbinu na kukuza uchumi hasa katika sekta
ya elimu ambapo karibu kila kata ina shule ya sekondari.
Aidha ameongezea kuwa
kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita serikali imetoa Zaidi ya bilioni
58 kwa ajili ya kuboresha ujenzi wa miundo mbinu mbali mbali hali ambayo
imesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa kibondo kwa kiasi kikubwa.
Katika hatua nyingine kiongozi wa mbio za
mwenge wa uhuru kitaifa Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava amewataka viongozi katika
wilaya ya Kibondo kusimamia vyema fedha zinazoletwa na serikali hasa katika
sekta ya elimu, afya, maji na barabara ili kukuza uchumiwa nchi na jamii kwa
ujumla.
Kwa muujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 14,2024 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma alipoupokea mwenge Mwenge huo wilayani Uvinza ukitokea mkoani Katavi
alibainisha kuwa miradi (83) mkoani kigoma itapitiwa na mwenge wa uhuru huku
ikiwa Jumla ya Miradi kumi(10) itawekewa Mawe ya Msingi, mitatu(3)
itafunguliwa, 27 itazinduliwa, 24 itatembelewa na kukaguliwa huku miradi
19 itahusisha ugawaji wa Vifaa kwa vijana wajasiriamali na misaada kwenye shule
na vituo vya kulea watoto wenyemahitaji maalum.
Mwandishi; James Jovin
0 Comments