Mwandishi wa habari na kiongozi wa radio Bw. Charles Makoto anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo akishukiwa kupinga sheria (Rebellion).
Tukio hilo limetokea leo asubuhi tarehe 2 Septemba mwaka huu, ikitajwa kuwa Polisi zaidi 20 waliizunguka nyumba yake iliyopo Tarafa ya Mtimbuzi Jijini Bujumbura na kumtia mbaloni.
Hata hivyo sababu hasa za kukamatwa kwa Mwanahabari huyo bado hazijawekwa wazi na jeshi la Polisi la nchi hiyo huku wakiahidi kutoa taarifa zaidi hapo baadae, ingawa taarifa zisizo rasmi zinasema amepinga sheria (Rebillion)
Charles Makoto ameingoza radio isanganiro kwa kipindi cha miaka 4, huku Radio hiyo ikitajwa kuwa miongoni mwa radio zinazosikilizwa zaidi nchini Burundi, pia ni miongoni mwa radio 3 zilizowahi kufungiwa kwa miaka 5 zikishukiwa kupinga muhula wa 3 wa Hayati Rais Pierre NKURUNZIZA.
Tarehe 14 August 2024 mwandishi na mtangazaji Floriane IRANGABIYE BUHA aliyekuwa ameshikiliwa Gerezani kwa kipindi cha miaka 2 nchini humo aliachiliwa huru baada ya mashirika ya haki za binadamu na waandishi wahabari kupinga unyanyasi huo
Imeandikwa na : David NDEREYIMANA
0 Comments