Mwenyekiti wa Wavuvi Kibirizi Mkoani Kigoma Paul Samwel amesema hatua iliyo chukuliwa na Serikali kufunga Ziwa Tanganyika imeweza kutoa matokeo chanya kwa wavuvi.
Mwenyekiti huyo amesema hayo septemba 12,2024 mkoani Kigoma baada ya mchakataji wa dagaa mwalo wa Katonga ziwa Tanganyika Zena Masoud kuchakata dagaa tani 1 baada ya ziwa kufunguliwa.
Aidha bw. Paul Samwel
ameongeza kuwa kwasasa wanachoendelea kupambana nacho ni kuboresha uhifadhi wa
mazao yanayo tokana na uvuvi na masoko ya ndani na nje ya nchi ili
kuleta uchumi wenye tija.
Ziwa Tanganyika lilifungwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Mei 15, 2024 na kufunguliwa August 16 na waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Hamis Ulega ,hali iliyorejesha tena matumaini kwa wavuvi wa ziwa hilo .
Awali,mwaka 2023 kulikuwa na
ukosefu wa dagaa na samaki kabla ya ziwa kufungwa, huku upatikanaji wa samaki na dagaa ukiwa wa bei kubwa kufikia elfu 55 hadi elfu 60 kwa kilo moja kutoka elfu 10 ya mwanzo , ambapo kwa sasa zinapatikana kwa bei kati ya elfu 20 hadi elfu 22 .
0 Comments