Lebanon yathibitisha ongezeko la vifo milipuko ya vifaa vya mawasiliano


Wizara ya afya nchini Lebanon imethibitsha ongezeko la vifo  takribni 20 na wengine wasiopungua 450 kujeruhiwa  katika ya shambulio lililosababishwa na mlipuko uliotokana na vifaa vya mawasiliano ya mkononi yaani simu huku wizara hiyo ikitahadharisha  hali kuwa mbaya zaidi  .

Taarifa hiyo imetolewa   siku ya  jumatano , 18,2024 na kusema kuwa idadi kubwa ya majeruhi imeongezeka kutokana na mlipuko huo unaohusishwa na  mgogoro kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah unaoendelea .

Siku ya Jumanne, vifaa vya mawasiliano ya ujumbe vya pager vililipuka na kuwauwa watu 12, wakiwemo watoto wawili, na kuwajeruhi wengine karibu 3,000.

Kwa upande wa jeshi la Israel (IDF) haijatoa taarifa yoyote kuhusu milipuko hiyo, huku waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant akisema kuwa nchi yake itafungua awamu mpya ya vita na wanajeshi wake waliohamia kaskazini mwa Lebanon kutoka eneo la Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC  limesema Japan imekana  kutengeneza vifaa vya maongezi vilivyolipuka Lebanon,vya Kampuni ya kutengeneza ''walkie-talky'  na kudai kuwa iliacha kutengeneza   vifaa hivyo vya mawasiliano vyenye nembo yake iliyolipuka nchini Lebanon kwa muongo  mmoja uliopita.

Hiyo ni kampuni ya pili ya bara la Asia kukumbwa na visa vya milipuko nchini Lebanon wiki hii, baada ya milipuko ya maelfu ya ''pager'' inayohusishwa na kampuni ya Taiwan ya Gold Apollo kuua takriban watu 12 na kujeruhi zaidi ya 2,000.


Wakati huo huo  pia shirika la BBC rimeripoti, raia mmoja  wa Israel amekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika njama na  Iran ya kumuua Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu, idara za usalama za Israel zimesema.

 Polisi wa Israeli na ujasusi wa ndani walisema mtu huyo alisafirishwa kwa magendo mara mbili hadi Iran na kupokea malipo ya kutekeleza "misheni" hiyo.

Katika taarifa yao ya pamoja, walisema mshukiwa huyo alikuwa mfanyabiashara ambaye alikuwa akiishi Uturuki na alikuwa na washirika wa Uturuki ambao walimsaidia kuingia Iran.

Taarifa hiyo inakuja kukiwa na uhasama kati ya Israel na Iran tangu kuanza vita vya octoba 7,2023 kati ya Israel na kundi la wanamgambo Hamas.

Mwandishi: Jenipha Sanga na Ramadhani Zaidy

Mhariri:Abel Mahenge 




Post a Comment

0 Comments