Mabalozi
wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Burundi leo anaungana na kutembelea kambi
ya wakimbizi wa Burundi na DRC wanaoishi nchini Tanzania na kuzindua mradi
wa pamoja unaovuka mpaka wenye lengo la kuwezesha wakimbizi kupata huduma hata wanaporejea
nchini mwao.
Tukio
hilo limefanyika leo katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma
yenye zaidi ya wakimbizi wa Burundi pamoja na DRC
Akizungumza
katika kikao cha pamoja cha wakimbizi, UNHCR, wadau na uongozi wa serikali
ngazi ya mkoa na wizara za mambo ya nje na mambo ya ndani, Balozi wa Umoja wa
Ulaya nchini Tanzania Bi. Christine Grau amesema Umoja wa Ulaya utaendelea
kutoa misaada kwa wakimbizi na kwamba tayari imetenga kiasi cha Euro milioni 3
kwa ajili ya wakimbizi wa DRC waishio Nyarugusu huku akitangaza pia kuwa kiasi
euro milioni 6 nyingine zimetengwa na umoja huo nchini Ubelgiji na zitatumika
kutoa huduma kwa wakimbizi nchini Tanzania.
Kwa
upande wake Balozi wa umoja wa Ulaya nchini Burundi Bi. Elizabetta Pietrobon
ameeleza kuwa mradi uliozinduliwa ambao ulianza october 2023 una thamani ya
Euro milioni 40 na inalenga kuwasaidia wakimbizi kupata huduma ndani ya kambi
na baada ya kurejea ikiwemo kuwapatia vitambulisho vya uraia, vyeti vya
kuzaliwa, elimu, na ndoa
Pamoja
na ahadi hizo wakimbizi kutola Burundi na DRC hawajaonesha kuridhishwa na ahadi
hizo huku wakisisitiza kuboreshwa kwa huduma ndani ya kambi na nchini Burundi,
huku wakisisitiza kupewa fursa ya hifadhi nchi ya tatu
Pamoja na madai hayo serikali ya Tanzania kupitia kwa mkurugenzi wa huduma za wakimbizi Bw. Sudi Mwakibasi pamoja na mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye wametoa wito kwa wakimbizi hususani wa Burundi kurejea na kwamba mradi wa Umoja wa Ulaya utakuwa na thamani rndani ya Burundi na si ukimbizini Tanzania
Mheshimiwa Andengenye amesisitiza kuwa ni wakati wa Wakimbizi hususani wa Burundii kuamua kurejea kwao kushiriki shughuli za maendeleoo na kusaidia Watoto wao kuishi na kuhudumiwa na taifa lao
Wakati
Tanzania ikihimiza wakimbizi wa Burundi kurejea, na wakimbizi wenyewe
kulalamikia ualama nchini Burundi, Mkurugenzi wa idara ya wakimbizi nchini
Burundi Bw. Nestory Bimenyimana ameeatoa hofu warudi kuwa Burundi kuna usalama
wa kutosha na huduma za kijamii zimeimarishwa
Bw.
Bimenyemina amebainisha kuwa kila mkimbizi anayerejea Burundi bila kujali umrii
anapewa kiasi cha dola 220 zinazomwenesha kuanzisha Maisha mapya huku
akisisitiza kuwa suala la usalama ni moja ya vipaumbele vya serikali Pamoja na
wadau wakiwemo Umoja wa Ulaya na Umoja wa mataifa.
Kwa
mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania Kambi ya Nyarugusu ina jumla
ya wakimbizi 135, 038 kati yao raia wa DRC ni 87,396 na Warundi ni 47,500
pamoja na waomba hifadhi kutoka Kenya, Uganda, Sudani Kusini, Somalia, Zimbabwe
na Rwanda wapatao 142 ambao hawajakubaliwa kuwa wakimbizi nchini Tanzania
0 Comments