Marekani yakataa ombi la Ukraine kutumia Silaha za masafa mrefu.

Waziri wa ulinzi wa marekani Lloyd Austin amekataa na kuondoa ombi la kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu za marekani kuyalenga maeneo ya ndani ya Urusi.

Waziri Austin ametoa kauli hiyo Septemba 7, 2024 wakati wa kuhitimisha mkutano wa wadau wa kimataifa wa waounga mkono Ukraine uliofanyika nchini Ujerumani katika kituo cha anga cha Marekani na kusema kuwa matumizi ya silaha hizo haziwezi kubadilisha muelekeo wa vita hiyo kwa mujibu wa DW.

Kwa upande mwingine waziri Austin amesema kuwa Washington na washirika wake wataendelea kutoa msaada mkubwa kwa Ukraine katika kupambana na uvamizi wa Urusi na kutanga msaada mwingine wa dola milioni 250.

Awali rai wa Ukraine volodmyr zelensky aliwasilisha ombi la kupatiwa na kuruhusiwa kutumia silaha za masafa marefu kuyalenga maeneo ya ndani ya urusi ili kukabiliana nja uvamizi wa nchi.

Mkutano wa wadau wa kimataifa wanaounga mkono Ukraine unaongozwa na waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin kwenye kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ramstein iliyoko kusini magharibi mwa mji wa Frankfurt Ujerumani.

Mwandishi; Ramadhani Zaidy

Post a Comment

0 Comments