Marekani imesema kupitia Kamandi yake ya Uratibu Barani Afrika septemba 16,2024 imemaliza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger na mchakato huo ulifanyika kwa awamu, maamuzi hayo yanajiri baada ya serikali ya kijeshi ya Niger mnamo mwezi Aprili iliagiza Marekani kuondoa wanajeshi na watumishi wengine wapatao 1,000 nchini humo.
Kwa muongo mmoja uliopita, wanajeshi wa Marekani wametoa mafunzo kwa vikosi vya Niger na kusaidia kukabiliana na ugaidi wa makundi ya Dola la Kiislamu na al Qaeda katika eneo hilo.
Awali,kabla ya mapinduzi nchi ya Niger ilikuwa mshiriki mkubwa wa Marekani katika vita dhidi ya uasi katika ukanda wa Sahel, na kusababisha vifo vya maelfu na wengine mamilioni kuyakimbia makazi yao.
Tangu kupinduliwa kwa rais Mohamed Bazoum, utawala wa kijeshi, chini ya uongozi wa jenerali Abdourahmane Tchiani,umekuwa na uhusiano baridi na nchi za magharibi, ikiwemo Mkoloni wake wa zamani Ufaransa .
Mwandishi; Shukuruimana Revokatus
0 Comments