Rais wa marekani Joe
Biden pamoja na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer wameahirisha maombi
ya Ukraine kutumia silaha za masafa
marefu zinazotolewa na nchi za Magharibi katika vita dhidi ya Urusi.
Uamuzi huo umetolewa siku
ya ijumaa ya September 13,2024 katika
kikao kilichofanyika ikulu ya White House mijini Washington Marekani na kusema kulikuwa na majadiliano ya mda mrefu juu ya uamuzi huo.
Aidha waziri mkuu wa
Uingereza Keir Starmer ameongeza kuwa nchi za Ulaya ya magharibi pamoja na Marekani zipo kwenye mkakati wa kutatua mzozo unaoendelea kati ya Ukraine na Urusi.
Awali rais wa Urusi
Vladimir Putin alitoa onyo juu ya mpango wa nchi za magharibi pamoja na
marekani juu ya mpango wa matumizi ya silaha hizo na kusema kuwa hatua hiyo
haiwezi kupunguza mzozo kati yake na Ukraine.
Katika juma liliopita
rais wa Ukraine volodymyr Zelensky aliwasilisha maombi ya kutumia silaha za
masafa marefu za Ulaya ya Magharibi pamoja na marekani kwa mara nyingine katika
vita dhidi ya Urusi.
Mwandishi; Ramadhani Zaidy
0 Comments