Mbivu ,Mbichi Taifa Stars ,Guinea kesho.

          Taifa stars wakiwa mazoezini Ivory coast TFF

 Timu ya Taifa Stars inayowania kupata nafasi ya kufuzu kushiriki Afcon 2025 imeendelea kujinoa katika uwanja wa mazoezi wa Yamoussoukro,Ivory coast kuikabili Guinea ikiwa ni mchezo wao wa pili katika kundi H utakaopigwa kesho Septemba 10.

Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF,Athuman Nyamlani amesema maandalizi yapo vizuri na wanategemea kupata matokeo mazuri kwakuwa kikosi kinawachezaji wenye uzoefu wa michuano mikubwa  .

 “mashabiki na wapenzi wa soka wanapaswa kutambua mpira unamatokeo matatu kushinda,kusuluhu,na kufungwa japo sisi tunategemea kupata matokeo mazuri  hivyo wajitokeze kwa wingi kuifuatilia na kushangilia timu yao”


Awali Naibu waziri wa Michezo na burudani Mh;Hamisi Mwinjuma amesema serikali inafanya juhudi katika sekta ya michezo lengo  kuongeza morali kwa wachezaji wetu ilikuendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania na kutengeneza ushindani wa ligi.

 "Raisi samia amenituma kuiwakilisha serikali hapa Ivorycoast na kutengeza morali kwa vijana wetu kwakuwa wachezaji wetu wanatambua kipi tunahitaji”.

Ikumbukwe kuwa Timu ya  Taifa ,Taifa stars ilifuzu kwa mara yakwanza mwaka 1980, badae 2019 na 2023 ambapo wakifuzu mwaka huu itakuwa mara yao ya nne.






Mwandishi: Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments