Mbunge wa Muhambwe aunga mkono juhudi za Rais Samia

Mbunge wa jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo mkoani Kigoma amegawa majiko ya gass yapatayo 200 kwa wajasiliamali, mama ntilie na baba ntilie katika kata zote 19 zinazounda jimbo hilo kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kutunza mazingira na kupunguza ukataji wa mito ovyo.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa majiko hayo mbunge wa Jimbo la Muhambwe Dr. Florence Samizi amesema kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha ifikapo 2033 asilimia 80 ya watanzania wote wawe wanatumia nishati safi na salama ya kupikia 

Aidha amesema kuwa yeye kama mbunge wa jimbo la Muhambwe hana budi kuunga mkono jitihada za rais Samia Suluhu Hassan katika malengo ya serikali ya  kutunza mazingira na kuhakikisha jamii inaishi mahali salama lakini pia vizazi vjavyo kwa ujumla

Kwa upande wao baadhi ya wajasiliamali na mama lishe waliopokea msaada huo wa majiko ya gass wameshukuru kwa msaada huo na kwamba itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharibifu wa mazingira katika mazingira yao.

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Muhambwe Dr. Florence Samizi amesema kuwa nishati ya kuni imekuwa ikisababisha kwa kiasi kikubwa madhara kwa binadamu na viumbe mbali mbali hivyo mpango wa kusaidia wananchi kutumia majiko ya gass ni mkombozi kwa jamii ya watanzania.  

Tanzania chini ya maelekezo ya Rais Samia Suluhuu Hassan imeweka mkakati wa kuhakikisha kila mtanzania anatumia nishati mbadala kama sehemu ya mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Mwandishi: James Jovin

Mhariri: Prosper Kwigize 

Post a Comment

0 Comments