Miaka 60 ya Jeshi la Polisi Rais Samia Mgeni rasmi

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Miaka 60 ya Jeshi la Polisi itakayofanyika katika shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro septemba 17,2024.


Taarifa hiyo imetolewa  na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna wa Polisi, David Misime wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro  na kusema kuwa Jeshi hilo limetoa taarifa kuhusiana na maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi Tanzania iliyoambatana na  shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo upimaji wa afya kwa wananchi bure katika Hospitali kuu ya jeshi jijini Dar es Salaam na zahanati zote za jeshi zilizopo mikoa yote nchini.   


DCP Misime ameongeza kuwa mambo mengine yaliyofanyika katika maadhimisho hayo ni Pamoja na Jeshi la Polisi kushirikiana na Jamii katika michezo Pamoja na kutoa elimu juu ya kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Mwandishi;Ellukagha Kyusa

Post a Comment

0 Comments