Miamba ya soka England mchakamchaka majira ya joto.

Wakala wa Mshambuliaji wa Misri na timu Liverpool ya England Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 32, ameongeza uvumi kuhusu hatma ya mchezaji huyo ndani kikosi cha majogoo wa jiji la London kwa kutumia kauli ya hasira kwenye mitandao ya kijamii.

Mtendaji mkuu wa timu ya Liverpool Michael Edwards anaongoza harakati za klabu hiyo ya kumtafuta kiungo mpya wa kati kwenye usajili wa dirisha la majira ya joto litakapo funguliwa .

Arsenal the Guners na Chelsea “the blues” zinatarajia kumjuisha kwenye orodha yao ya wachezaji watakaowanunua katika dirisha la usajili majira ya joto mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswid Viktor Gykeres 26, litakapo funguliwa.

Chelsea na Tottenham bado wanavutiwa na mlinzi wa Lecce wa Denmark Patrick Dorgu,19 ambaye thamani yake ni takribani euro milioni 40.

Mchezaji wa kimataifa wa Hungary na timu ya Freiburg Roland Sallai mwenye umri wa miaka 27, amekataa ofa yakusaini na Leeds United ya pauni milioni 8.5 katika dirisha la usajili majira ya joto na kuamua kutimukia kwa miamba ya Uturuki Galatasary.

Mwandishi; Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments