Miamba ya soka England na harakati za kuboresha timu msimu wa joto.

Kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Jamal Musiala 

Timu ya majogoo wa jiji la London Liverpool wamepiga hatua katika juhudi za kunasa saini ya kiungo wa Bayern Munich Jamal Musiala mwenye miaka21, Huku klabu za Manchester City , Real Madrid na Paris St- Germain nao wakiwa katika msafara huo wa kumfukuzia mshambuliaji huyo wa Ujerumani.

The red Devels Manchester United wana matumaini ya kununua winga wa Paris St Germain Xavi Simons baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 21 ambaye kwasasa yuko kwa mkopo RB Leipzig kusema haoni mustakabali wa klabu hiyo ya Ligue 1.

Wakati huohuo man.united imewaorodhesha wachezaji safu ya ushambuliaji Jonathan David 24,wa Lille raia wa Canada , na Mshambuliaji wa Al-Ahli na Uingereza Ivan Toney 28, kama mbadala wa Joshua Zirkzee iwapo watashindwa kunasa saini ya Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 23 kutoka Bolgana.

Winga wa Pembeni wa PSG Xavi Simons  

Baada ya dili la Kuhamia AEK Athens kutibuka, Mshambuliaji wa “The blues “ Chelsea na Ivory Coast David Datro Fofana mwenye umri wa miaka 21 amefikia mkataba wa mkopo na klabu ya Uturuki Goztepe SK .

West Ham United wana nia ya kunasa saini ya mlinzi wa zamani wa Liverpool Joel Matip 33, kwa uhamisho wa bure kwani mlizi huyo raia wa Cameroon mzaliwa wa Ujerumani bado hana timu anayo itumikia.

Mshambuliaji wa Chelsea na Ivory Coast David Datro Fofana.

Manchester United na The Guners Arsenal wameshindwa kufikia mshahara ya pauni 220,000 kwa wiki anaouhitaji kiungo wa kati wa Ufaransa Adrieni Robiot mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mchezaji huru na kuamua kutangaza kusitisha harakati za kutaka kuinasa saini ya kiungo huyo wa kati.

Mwandishi; Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments