Morogoro kutoa elimu ya mpiga kura.


Ikiwa imesalia miezi miwili kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji Novemba 27 mwaka huu, halmshauri ya Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro imezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura.

Mkuu wa Wilaya Kilombero, Wakili Dunstun Kyobya amesema kampeni hiyo inayotambulika kama Elimu ya mpiga kura imezinduliwa katika halmshuuri hiyo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa zoezi la uandikishaji katika daftafi la kidumu la mpiga kura linalotarajiwa kuanza octoba 11_octoba 20 mwaka huu katika eneo hilo. 

Kyobya amewaomba wasanii, viongozi wa dini na viongozi wa kimila kutoa hamasa kwa wananchi kuona umuhimu wa kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura kwa viongozi wanao wahitaji zoezi hilo litakapo anza.

Mkurugenzi mtendaji halmshuuri ya Ifakara Mji, Zahara Michuzi amesema wameanza kutoa elimu kwa makundi maalumu na kutoa miongozo kwa viongozi wa vijiji,vitongoji 

Mwandishi; Ellukagha Kyusa


Post a Comment

0 Comments