Mpango aitaka "UNFCCC" kuja na majibu mabadiliko tabianchi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philipo Mpango 

                     (Picha DAILNEWS)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Philipo Mipango ameitaka kamata ya kudumu ya Fedha ya mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) kuja na mapendekezao yatakayojibu changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt . Mpango amesema  hayo  leo septemba 2 ,2024 wakati akifungua Jukwaa la 24 na mkutano wa 35 wa kamati ya kudumu wa fedha ya mkataba wa umoja wa  mataifa wa mabdiliko ya tabianchi, linalofanyika katika ukumbi wa kimafaifa wa mikutano ( AICC) Jijini  Arusha.

Akieleza mikakati ya Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Dkt. Mpango amesema serikali ya Tanzania imekusudia kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ili kupunguza matumizi ya kuni  ambao ni moja ya sababu ya mabadiliko ya tabianchi  nchini na kuhakikisha  kufikia 2033 asilimia 80 ya watanzania  wanatumia nishati safi.

Aidha Dkt.Mpango ameongeza kuwa  serikali ya Tanzania imetoa Fedha zitakazo weza kusaidia kupambana na adhari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo ambao ni wa mara ya kwanza kufanyika nchi Tanzania unatarajiwa kudumu kwa siku mbili  ni maandalizi ya  mkutano wa COP29 unaotarajiwa kufanyika Novemba 11 hadi 22, 2024 mjini Baku, nchini Azerbaijan.

 Kamati ya kudumu ya fedha ya umoja wa mataifa ni moja ya kamati chini ya mkataba wa umoja wa mataiafa wa  mabadiko ya tabianchi iliyoundwa katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa COP16 wenye lengo lakuwezesha upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa shughuli za mkataba na kamati  ambayo ina jumla ya wajumbe 32 kutoka nchi zinazoendelea na zilizoendelea ambao ni mwanachama wa mkataba huo.

Imeandikwa na: Ramadhan Zaidy

Post a Comment

0 Comments