Mafuriko yaliyosababishwa na kuvunjika kwa kingo za bwawa ,yamewaua watu 30 na kuharibu makumi ya nyumba huko Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria,
Msemaji wa Wakala wa Kitaifa wa Usimamizi wa Matukio ya Dharura,bw. Ezekiel Manzo amesema kwamba idadi ya watu waliofariki imefikia 30, na watu milioni moja wamepoteza makaazi yao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la umoja wa mataiafa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Nigeria kupitia mtandao wake wa X imesema hayo ni mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka 30 .
Serikali ya jimbo hilo imesema bwawa hilo lilivunjika kingo na kuhama mwelekeo wake kutokana na mvua kubwa iliyonyesha isivyokawaida.
Mafuriko ya sasa yanakuja
karibu miaka miwili, tangu mafuriko mabaya zaidi ya Nigeri yalioua watu zaid ya
600 kote nchini humo.
Mwandishi: Abel Mahenge.
0 Comments