Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg.Godfrey Eliakimu Mzava amefanya uzinduzi wa nyumba ya watumishi katika shule ya sekondari Mwilamvya mpya iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani
Kigoma .
Uzinduzi huo umefanyika leo Septemba 18, 2024 katika shule hiyo huku kukiambatana na zoezi la upandaji miti na kusema nyumba hiyo itumike kwa matumizi ya walimu ambao hawana makazi karibu na eneo la kazi.
“ nyumba hii ianze kutumika mara moja ili kupunguza kero za umbali na kuleta thamani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt. Samia maana hatuwezi kuzindua nyumba halafu isitumike,
nyumba hii itumike kwa walimu waliopo au walimu wa ajira mpya” Amesema Mzava.
Aidha mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mwilamvya Godwin Baltazari ameshukuru na kusema kuwa ufunguzi wa nyumba hiyo utawasaidia walimu waliopo mbali na eneo la shule hivyo kutimiza majukumu yao kwa wakati sahihi.
“Uzinduzi huu utawasaidia walimu wanaoishi mbali kutimiza majukumu yao kwa wakati maana walimu wakikaa mbali na shule wanashindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati sahihi''Amesema mwalimu Godwin.
Mwandishi; Sharifat Shinji.
Mhariri: Ellukagha Kyusa.
0 Comments