Ndege ya Rais wa Venezuela yashikiriwa nchini Marekani


Ndege ya Rais wa Venezuela, Nicolaus Maduro  iliyokamatwa Marekani. (picha kutoka globalpblishers)

Marekani imekamata Ndege ya Rais wa Venezuela Nicolaus Maduro ikidai ilinunuliwa kinyume cha sheria kwa kiasi cha pesa za marekani Dola milion 13 na kutoroshwa nje ya nchi.

Ikiripotiwa leo Septemba 03,2024 na globalpublishers kuwa wizara ya sheria ya Marekani imesema Ndege hiyo aina ya Falcon 900EX ilikamatwa katika jamhuri ya Dominika  Septemba 02,2024 na kuhamishiwa jimbo la Florida nchini marekani.

Data za ufatiliaji chini ya Maafisa wa Marekani zinaonesha Ndege hiyo iliondoka kwenye uwanja wa Ndege wa La Isabela karibu na mji mkuu wa Santo Domingo siku ya jumatatu na kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale huko Florida baada ya masaa machache badae.

Hata hivyo Maafisa hao wamebainishakuwa Ndege hiyo imekamatwa kwa tuhuma ya ukiukwaji wa sheria  ya ukiukaji wa udhibiti wa mauzo ya nje na sheria huku wakiongezea kuwa uchunguzi ulifanyika na kugundua kuwa Bw. Maduro anahusika na ukiukaji  wa sheria hiyo kwa kutumia kampuni ya Shell ya Caribbean kwa ununuzi haramu wa Ndege hiyo mwishoni mwaka 2022.

Serikali ya Vernezuela inaishutumu Marekani kwa unyakuzi wa Ndege hiyo na kudai kuwa sawa na kitendo cha uharamia huku wakipanga kuchukua hatua zozote za kisheria kufatia kwa kitendo cha kushikiriwa kwa Ndege hiyo.

Kwa mujibu wa chabisho la bbcswahili mgogoro huo wa ndege umeanza zamani  licha ya kufanya mazungumzo  lakini hatua za uchunguzi zilibainika mwezi mmoja tu baada ya uchaguzi wa Julai 28, ambapo Maduro alitangazwa mshindi bila kuonyesha rekodi za upigaji kura na licha ya madai ya udanganyifu kutoka kwa upinzani.

Hata hivyo serikali ya Rais Joe Biden haitambui ushindi wa Maduro, juu ya ununuzi wa ndege hiyo baada ya mgombea wa upinzani, Edmundo González, na kiongozi María Corina Machado, kuchapisha 81.7% ya ushindi ambao unaunga mkono upinzani.

Imeandikwa na; Shukuruimana Revokatus.

Post a Comment

0 Comments