Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameomba radhi kwa Waisraeli kwa kushindwa kuwarudisha mateka sita waliopatikana wameuwawa huko Gaza, siku ya jumamosi .
Kauli yake inakuja baada ya maandamano Makubwa ya barabarani katika miji mbalimbali ikiwemo Jerusalemu na Tel Aviv yakimshinikiza waziri mkuu Netanyahu kukubaliana na makubaliano ya Hamas ili kurejesha mateka 101 waliosalia katika mikono wanamgambo wa Hamas.
Hata hivyo serikali ya Benjamin Netanyau ilikimbilia mahakamani kupinga maandamano na Mgomo uliongozwa na chama cha wafanyakazi wa nchi hiyo ambao ulianza septemba 2, 2024 saa 12: 00 za Asubuhi na kusamba nchi nzima ikiwemo jiji la Jerusalemu na Tel aviv
Wakati mgomo huo wa siku moja ukiendelea, mahakama ikaamuru mgomo huo kusitishwa kwani haukulenga maswala ya uchumi au utetezi wa wafanyakazi kama ulivyo wajibu wa chama cha wafanyakazi .
Wakati hayo yakiendelea huko Israel Uingereza imetangaza itasitisha baadhi ya mauzo ya silaha kwa Israel, waziri wa mambo ya nje David Lammy BBC amesema hayo jumatatu tarehe 2 septemba mwaka huu.
Bw Lammy alisema uamuzi huo unafuatia mapitio ya leseni za mauzo ya silaha za Uingereza, ambayo iligundua kuwa kuna hatari ya wazi kwamba zinaweza kutumiwa kufanya ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu".
"Ni kwa masikitiko kwamba nalijulisha Bunge leo tathmini niliyoipata inaniacha siwezi kuhitimisha kitu kingine chochote isipokuwa kwamba kwa uuzaji wa silaha za Uingereza kwa Israeli, kuna hatari ya wazi kwamba zinaweza kutumika kufanya au kuwezesha kosa kubwa- ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu."
0 Comments