Ngorongoro yarejeshwa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametangaza jumla ya vijiji 12, 333, mitaa 4,269 na vitongoji 64, 274 vitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa  unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Septemba 17,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kuongeza kuwa kwenye orodha hiyo yamejumuishwa maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa tangazo la serikali  673 na 674  ambayo pia yalihusisha tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Mchengerwa pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo na kuunda serikali ya kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mustakabali wa maendeleo.

Katika kipindi cha miaka ya uhuru yalikuwepo makundi matatu ya serikali za Mitaa miongoni mwao ni zile zilizoundwa chini ya sheria namba 72 ya mwaka 1926 zilizo kuwa 47 pia chini ya sheria namba 333 ya mwaka 1952 zilikuwa 9 kwa mijini na 10 kwa vijijini.

Aidha kundi la tatu lilikuwa ni la manispaa ya Dar Es Salaam iliyo undwa na sheria namba 105 ya mwaka 1946 na mwaka 1962 sheria namba 333 ulirekebishwa kwa kuondoa mamlaka za wenyeji na mwaka 1963 sheria namba 13/62 ilipitishwa kusitisha utawala wa machifu nchini.

Mwandishi; Shukuruimana Revokatus

Post a Comment

0 Comments