Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis amelaani na kukosoa hali ya machafuko inayoendelea kuongezeka Lebanon akisema kuwa kupitia machafuko hayo Israel imeendelea kuua mamia ya watu kusini mwa Lebanon.
Papa Francis amesema hayo septemba 25,2024 huku akisistiza jumuia ya
umoja wa mataifa kufanya juhudi ya kusitisha mgogoro huwo ili kuokoa maisha ya
raia wa nchi hizo.
Awali katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Gutteres akinukuliwa na DW
katika mkutano wa 76 wa umoja wa mataifa uliofanyika New York marekani septemba
24,2024 na kusema watu wa Lebanon, Israel
na ulimwengu mzima ni lazima wahakikishe kuwa Lebanon haigeuki na kuwa Gaza
nyingine.
Usiku wa septemba 24,2024 Jeshi la Israel (IDF) limekiri na kusema
linafanya mashambulizi mengi ya anga kusini mwa Lebanon na katika bonde la
mashariki la Bekaa baada ya kundi la Hezbollah kufyatua kombora la masafa
marefu hadi mji wa Tel Aviv.
Shirika la habari la serikali ya Lebanon limeongeza kuwa roketi mbili zimeanguka
katika kijiji cha Maaysra, chenye idadi kubwa ya Washia katika eneo la milima
la wakristo lililoko Keserwan kiasi cha kilometa 25 kutoka mji mkuu.
Hii ni mara ya kwanza kwa kundi la Hezbollah kudai kufanya
shambulizi la kombora la masafa marefu tangu vita vyake na Israel vilipoanza
baada ya kundi la Hamas kufanya shambulizi kubwa nchini Israel mnamo Oktoba
7 2023.
Mwandishi; Ramadhan Zaidy
Mhariri; Eunice Jacob
0 Comments