PM awataka wazazi Geita kuzingatia malezi Yenye maadili.


Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassimu Majaliwa amewataka viongozi wa dini ,wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili ya kiroho ili kuliepusha vitendo viovu katika taifa.

Waziri mkuu amemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tnazania Dkt.Samia Suluhu Hssan katika sherehe za Maulid Kitaifa Mkoa wa Geita leo septemba 16,2024 na kusema wajibu wa malezi na ulinzi wa taifa ni jukumu la kila mwananchi .

"Nitoe rai kwa wazazi na walezi tulioko hapa tunawajibu wa kuhakikisha tunawalea watoto katika maadili ya taifa letu kupitia mafundisho ya dini ili kuepusha taifa na matendo maovu na kila mwananchi anawajibu huo"Amesema Majaliwa.

Aidha  waziri mkuu Majaliwa amesema kuwa ipo mitaala ya elimu ya kislamu na kikristo mbayo itamfanya mwanafunzi kupata maadili mema awapo shuleni na nyumbani sanjari na kumwongezea ufaulu katika masomo yake ya mwisho.

Hata hivyo amewaomba wasimamizi wa elimu ngazi ya wilaya wakiwemo wakurugenzi kuandaa walimu wabobezi wa elimu ya kiroho ili kutengeneza kizazi kinachofuata misingi ya imani.

Ikumbukwe kwamba Sherehe za Maulid huadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) na kuunganisha waislam wote ulimwenguni kuadhimisha kila mwaka ifikapo   mwezi wa Rabiul Awwal kalenda ya kiislamu ambapo siku hii ilianza rasmi kusheherekewa katika karne ya 12.

Imeandikwa; Abel Mahenge na Shukuruimana Revokatus.

Post a Comment

0 Comments