Maandamano ya CHADEMA, Polisi yawatia nguvuni wandishi wa Habari.

Mwandishi wa habari wa Mwananchi na Mpigapicha wa Gazeti la Nipashe, wamekamatwa na polisi wakati wakitimiza majukumu yao kazi katika eneo la Buguruni na Ilala Jijini Dar Es Salam ambako viongozi na wanachama wa CHADEMA walikusanyika kwa lengo la kuandamana.

Mpigapicha Jumanne Juma wa Gazeti la Nipashe baada ya kukamatwa alipelekwa katika Kituo cha Polisi Buguruni, ambako alihojiwa na kuachiwa baada ya saa moja kupita ameelezea namna jinsi polisi walivyomkamatana na kumhoji maswali ya kwa nini wanapiga picha za maandamano.

"Nilivyofika nilikwenda kujitambulisha kwa kiongozi wa Askari waliokuwepo lakini baada ya muda walituzunguka wakatukamata mimi na mwandishi wa mwananchi, tukapelekwa kituoni tukahojiwa, baadaye wakatupeleka kwa Mkuu wa Kituo ambaye aliwaambia kama mmewahoji na hawana madhara waachieni, ndipo tunaaachiwa"amesema Jumanne.

Aidha, Mwananchi Communication Limitet(CML) imeripoti kuwa Lawrence Mnumbi ambaye ni mpiga picha wa chombo hicho cha habari bado ameshikiriwa na jeshi la polisi licha ya kumwachia miongoni mwa wapiganpicha wa chombo hicho Michael Mtenange aliyekamatwa bugruni pamoja na mpiga picha wa nipashe.

Sambamba na hayo jeshi la polis nchini limemethibitisha kwa kuwakamata viongozi wa chama upinzani nchini CHADEMA,amabao ni mwenyekiti, Freeman Mbowe na Makamu wake Tundu Lissu waliokusudia kufanya maandamano ya amani katika Jiji la Dar Es  Salam.

Hii si mara ya kwanza kwa mwandishi wa habari  kukamatwa ikumbukwe kwamba miezi michache iliyopita waandishi wahabari kadha walikamatwa jijini mbeya wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi  hivyo kupelekea mijadala mikubwa 

Ifahamike mkurugenzi wa halmashauri ya Temeke Lusabilo Mwakabibi, kuwakamata  waandishi wa habari wawili walioitwa na wafanyabiashara wa soko la mbagala ambapo walikuwa wakiwasilisha hoja zao kwa mkurugenzi hatua ambayo mkurugenzi huyo aliwaweka chini ya ulinzi hadi pale alipotamatisha mkutano wake kwa madai wamevamia mkutano, tukio ambalo lililaaniwa vikali na wadau wa habari.

Mwandishi; Abel Mahenge

Mhariri; Sharifat Shinji



Post a Comment

0 Comments