Rais Abdelmadjid Tebboune ashinda muhula wa pili Algeria.

                                           Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune (DW) 

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amechaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kwa kupata asilimia 95 ya kura baada ya uchaguzi uliofanyika siku Jumamosi, septemba 7,2024

Matokeo hayo yametangazwa jana jioni na mkuu wa tume ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo Mohamed Charfi.

Tebboune alitumia kampeni yake kuwahimiza wapigakura kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa mwaka huu akilenga kuifuta rekodi ndogo ya wapigakura katika uchaguzi uliomwingiza madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2019.

Bw. Charfi. alitangaza kuwa uchaguzi mwaka 2024 ulikuwa na ushiriki mdogo, wa   48.03%  licha ya kupanda kwa 11% ikilinganishwa na mwaka 2019 ambao ilikuwa  39.83%.uliompa ushindi  wa asilimia 58% Bw. Tebboune  huku mwaka huu  akipata asilimia 95% ya kura zote.  

Hata hivyo Wapinzani wa Tebboune  wamelalamikia uwepo wa hitilafu kwenye zoezi la kuhesabu na kujumlisha kura.

Tebboune mwenye umri wa miaka 78 alitarajiwa kuibuka mshindi wa uchaguzi huo kutokana na kampeni zake kuwa na ushawishi kwa raia wa taifa hilo  akichuana dhidi ya mgombea anayeegemea sera za dini ya kiislamu Abdelaali Hassani na msoshalisti Youcef Aouchiche.

Mwandishi: Ellukagha Kyusa

Post a Comment

0 Comments