Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan ameagiza uongozi wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kusimamia bei elekezi ya mazao na kutoa elimu kwa wakulima ili kuwaongezea maarifa ya biashara yenye tija na kuipatia serikali mapato.
Dkt, Samia amesema hayo septemba 25,2024 ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya kikazi ya siku tano mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi mkoani Ruvuma.
‘’wakulima wawezeshwe kuuza mazao kwa bei
elekezi yenye manufaa ambayo itawapa mapato ya kufuta jasho lao na kuhakikisha
wanarudisha gharama walizozitumia kulima na wabakiwe na faida kwaajili ya
mahitaji ya familia’’alisema Rais Samia.
Awali Waziri wa kilimo Mhe;Hussein Bashe(Mb) wakati akizungumza na wananchi amesema Serikali itahakikisha inatoa mwongozo wa mbegu za mahindi na kuingiza kwenye mfumo wa ruzuku huku akiahidi kuwachukulia hatua za kisheria wale wanao uza mbegu bandia.
Aidha Mhe; Bashe amesema mbegu hizo zitapatikana kwa namba wanayotumia wanunuzi wa mbolea ili kuondokana na uhujumu uchumi ndani ya taifa kwa lengo la wakulima nchini kununua mbengu zilizo kusudiwa kwa kilimo chenye tija.
‘’Kuanzia sasa mbegu zitakuwa zinauzwa na
karatasi maalumu ili mkulima anaponunua mahindi mfuko ule utawekwa namba ya kukwangua kama unavokwangua vocha na kukuletea
taarifa kwenye simu yako moja kwa
moja’’alisema Waziri Bashe.
Ni ziara ya kwanza ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo mkoani Ruvuma na viunga vyake ambapo Rais Dkt. Samia Suluh Hasan ameweka mawe ya msingi katika Ghala la nafaka Luhimba,pamoja na uzinduzi wa jengo la ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani humo.
Mwandishi; Shukuruimana Revokatus.
Mhariri: Eunice Jacob.
0 Comments