Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya mji Kasulu,Mwl. Vumilia Simbeye amewataka wakazi wa mji wa Kasulu kujitokeza kwa wingi katika
zoezi la uandikishaji wa wapiga kura wa serikali
za mitaa unatarajiwa kuanza tarehe 11 hadi 20 Octoba 2024.
Mwalimu
Simbeya amesema hay oleo septemba 26,2024 katika kikao na waandhishi wa
habari katika ofisi za halmashauri ya mji Kasulu wakati akitoa maelekezo ya
kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024.
“Maelekezo haya nayatowa siku 62 kabla ya
uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila mgombea pamoja na wapiga kura wanapata
haki na uchaguzi unafanyika kwa uwazi na
usawa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwana serikali” Amesema Mwalimu
Vumilia.
Aidha Mwalimu Vumilia ameongeza kuwa kabla
ya kuanza zoezi la uandikishaji Octoba 11,
mwaka huu wananchi watapewa maelekezo ya vituo vya kujiandikisha katika mitaa yao .
“tarehe 1 hadi 7 mwezi novemba zitakuwa
siku za kuchukua fomu za wagombea kwa wananchi wenye sifa, wkati huo tarehe 11 hadi 20 zoezi
la uandikishaji litakuwa linaendelea na kampeni zitaanza novemba 20 hadi 26 ,Ambapo tarehe 27
novemba mwaka huu utafanyika
uchaguzi wa serikali za mitaa” Amesema Mwalimu Vumilia.
Nao baadhi ya wananchi katika halmashauri ya mji Kasulu
wamesema kuwa wamejipanga vilivyo kuelekea uchaguzi huo, huku wakihimiza
uchaguzi wa kidemokrasia kwa wagombea na wasimamizi wa ucahaguzi ili kulinda amani ya eneo husika.
“tumejipanda vilivyo kuelendea uchaguzi wa
serikali za mitaa katika maeneo yetu lakini pia niiombe selikali kuzingatia demokrasia
ili kulinda amani na utulivu wa mji wetu” wamesema Baadhi ya wananchi.
Mchungaji kiongozi wa kanisa la anglikana na mwenyekiti wa baraza la cct kasulu mji Mch. Asheri Mageje (picha na Elukaga kyusa )
Kwa upande wa viongozi wa dini Kasulu ,wakiwakilishwa na Mchungaji Kiongozi
Kanisa la Anglican Wilaya ya Kasulu mji na
mwenyekiti Baraza la Kikristo Tanzania (CCT)
Wilaya ya Kasulu mji Asheri Mageje amewahimiza
wanasiasa kutunza Amani,Haki na uadilifu wa kila mwananchi .
“Nawashukuru viongozi wa Halmashauri kwa kuwashirikisha
wananchi kuelekea uchaguzi waserikali za mitaa ,Pia Nawaomba Wanasiasa tulinde Amani ya mji wetu
Kasulu tunapoelekea Zoezi la uandikishaji ,kampeni na uchaguzi Serikali ili kila mwananchi apate
haki yake kisheria “
Uchaguzi wa serikali za mitaa hufanyika
kila baada ya miaka mitano ambapo wananchi huchagua serikali itakayo waoongoza
wananchi wa mtaa husika katika kipindi cha miaka mitano ambapo uchaguzi wa
serikali za mitaa uliopita ulifanyika Novemba 2019.
0 Comments