Rais Samia awataka wananchi kuchagua viongozi bora serikali za mitaa

 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,  Samia Suluhu Hassani amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuchagua viongozi sahihi kwa maendeleo  ya nchi .

Rais Samia ameyasema hayo leo  Septemba 26  Wilayani ya Namtumbo Mkoani Ruvuma alipokuwa akizungumza na wananchi na kusisitiza  kuwa Ushiriki wa  kutosha  wa wanachi katika kuchagua viongozi bora  wa serikali za mitaa unawashirikisha  Katika kuleta  maendelo ya nchi.

“Mwanachi anawajibu wa kuchangua viongozi  bora, hili  ni jukumu la  kila Mtanzania hivyo tujitokeze kwa wingi ili kufanya maamuzi yaliyo sahihi ’’Rais Samia .

Aidha Rais Samia ameipongeza Wilaya ya  Namtumbo kuwa  miongoni mwa wilaya zinazozalisha  kwa wingi mazao  ya biashara ikiwemo,mahindi,Maharage pamoja na Kahawa inayoongoza kuliingizia  Taifa fedha za kigeni ambazo zinatumika kuleta maendeleo ya nchi.

Katika hatua nyingine Rais Samia akiwa katika kata ya Rwinga Wilayani humo amesema serikali ipo tayari kuwapa wanachi mbegu bora za mazao ili kuongeza uzalishaji ,na kusema kuwa serikali itaanza kuzalisha mbegu, ili kusaidia wakulima kufanya kilimo cha kisasa  ili kupata utoshelevu na ziada ya chakula nchini.

Rais  wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  yuko mkoani Ruvuma kwa  Ziara ya kikazi ya  siku 5,Ziara Hiyo imeanzia  Wilaya ya Songea ,Ikifuatiwa na Wilaya ya Nyasa ,na leo yupo Wilayani Namtumbo akiendelea na ziara yake wilayani Tunduru ambapo ziara hiyo  inatarajiwa kuhitimika septemba  28 mwaka huu.

Mwandishi: Shukuruimana Revocatus

Mhariri: Harieth Kamugisha  

Post a Comment

0 Comments