Ruto atetea serikali yake ya miaka miwili.


Rais wa Jamuhuri ya Kenya, William Ruto ametetea rekodi yake ya miaka miwili madarakani huku akibainisha kuwa hakuna serikali ya nchi hiyo iliyowahi kuweka mikakati madhubuti ya kuiendeleza Kenya.

Hayo yamesemwa Septemba 15,2024 kwenye mahojiano maalumu na DW yaliyo fanyika mjini Berlin nchini Ujerumani wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini humo. 

Aidha utetezi wa mkataba alio usaini Jumamosi iliyopita na Kansela Olaf Scholz wa ujerumani kwa lengo la kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wa Kenya na kuwasaidia wafanyakazi wenye ujenzi kupata nafasi za ajira nchini Ujerumani.

Hata hivyo alikuwa Berlin kushiiriki tamasha la wananchi wa ujerumani Burger Fest amabalo huandaliwa kila mwaka na ofisi  ya Rais wa ujerumani pamoja na kutia saini mkataba utakaowezesha maelfu ya wakenya walio na ujuzi kupata ajira nchini humo.

Pia alipo zungumuza malalamiko ya juu ya gharama kubwa za maisha na ukosefu wa ajira nchini Kenya alisema Serikali haaina mpinzani hata alipoingia madarakani aameweka mikakati ya kushughurikia changamoto zinazolikaabili Taifa hilo.

Kabla ya mkataba huo siku chache nyuma Kenya ilitia saini mkataba wa usambazaji wa umeme kupitia ushirikiano wa sekita binafsi na kampuni ya Adani ya India, Pamoja na benki ya maendeleo ya Afrika.

Mwandishi; Shukuruimana Revokatus

Post a Comment

0 Comments