Ruvuma kunufaika na huduma bora za afya.


Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama ameuhakikishia umma na wananchi wa mkoa wa Ruvuma kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendele na uboreshaji wa huduma za Afya ikiwemo upatikaji wa vifaa tiba pamoja na dawa.

Waziri Mhagama amesema hayo leo Septemba 20, 2024 baada ya kuwasili mkoani Ruvuma na kupokelewa na Mkuu wa mkoa huo Mhe. Ahmed Abbas.

Aidha Mhagama amesema Mkoa  wa Ruvuma utanufaika na ujenzi wa wodi maalum za watoto wachanga waliozaliwa na uzito pungufu (NCU) ili kufikia lengo la Serikali kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Kuhusu suala la lishe, Waziri Mhagama amesema Serikali inaendelea na zoezi la kutoa elimu kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ambao katika kila Kitongoji watakua Wawili (Wakike na Wakiume) watakaotoa elimu na huduma za kijamii za awali kwa wananchi.

Ziara ya Waziri Mhagama mkoani Ruvuma inafanyika siku chache kabla ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan itakayoanza Septemba 23,2024 mkoani humo.

Waziri Mhagama akiwa mkoani Ruvuma anatarajia kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Jimbo la Peramiho ikiwemo kukagua utoaji wa huduma kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (RRH), Kukagua utekelezaji wa mradi mpya (New OPD) pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Sekta ya Afya.

Mwandishi; Eunice Jacob

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments