Safu ya Taifa stars wakabidhiwa Guinea leo.

                       TFF

Washambuliaji wa timu ya Taifa Stars Waziri Junior, Clement Mzinze, na Cyprian Kachwele wanatariwa kuwa na jukumu muhimu ya kuongoza safu ya ushambuliaji katika mechi yao Dhidi ya Guinea itakayochezwa  leo septemba 10,2024  katika  dimba la Charles Konan Banny ulioko Yamoussoukro nchini Ivory Coast.

    Kulingana na taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka Afrika,     (CAF) Timu ya taifa ya Guinea imechagua kutumia uwanja Charles Konan Banny ulioko Yamoussoukro nchini Ivory Coast kwa mechi zake za nyumbani kutokana na ukosefu wa viwanja vyenye viwango vya CAF nchini humo .

Guinea wanaingia kwenye Mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa awali ugenini dhidi ya Dr Congo kwa kuruhusu kufungwa goli 1-0 katika uwanja wa Stade Des Martyrs, Kinshasa.

Taifa Stars  ambayo inahitaji alama tatu muhimu ili kufuzu kwa Afcon ya nne tangu mwaka 1980, walishindwa kutamba katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Ethiopia baada ya mechi  ya awali kutoka suluhu ya bila kufungana na kuambulia alama 1 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa ,Dar es salaam  septemba 4 mwaka huu.

Mashindano ya Afcon 2025, yanatarajiwa kuchezwa  Desemba 21,2025 hadi Januari 18,2026 nchini Morocco,ambayo itashirikisha timu 24, na taifa stars ipo kundi H wakiwa nafasi ya 2 na alama 1 pamoja na DR Congo inayo ongoza kundi kwa alama 6, Ethiopia alama 1 na Guinea wakiburuza mkia bila kushinda mchezo wowote hadi sasa.

Mchezo wa taifa stars na Guinea utachezwa saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki na ikiwa taifa stars itashinda itafikisha alama 4 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili ya kundi hilo 

Mwandishi:Eunice Jacob

Post a Comment

0 Comments