Serikali kuanzisha elimu ya watu wazima

                                                                                                                                        Picha: Mwananchi

Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema Halmashauri zote nchini zimeanzisha Idara pamoja na vitengo maalumu  vya elimu ya watu wazima walio na changamoto ya kutojua kusoma na kuandika.

Waziri Kipanga ameyasema hayo Bungeni September 4,2024 Jijini Dodoma wakati wa kujibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti maalumu Shally Raymond kwaajili ya kuwasaidia watu walio na changamoto hiyo.

Aidha mbunge huyo ameongeza kwa kuiomba serikali ifanye mkakati wa kuanzisha madarasa ya ziada ambayo yatatoa Elimu kwa watu wazima wasiojua kusoma na kuandika.

Serikali imeendelea kuimarisha elimu ya watu wazima kupitia programu mbalimbali zilizo chini ya sekta ndogo ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo.

Awali katika sensa ya watu na makazi mwaka 2022 ilionyesha idadi ya watu wasio jua kusoma wala kuandika nchini ni asilimia 17 ambayo bado ni asilimia kubwa kulingana na maisha ya karne ya sasa ,Pia katika  maboresho ya sera ya Elimu pamoja na mitaala iliyofanywa mwaka 2023 ililenga kutatua changamoto.

Imeandikwa na; Shukuruimana Revokatus

Post a Comment

0 Comments