Sheikh Mzee Motawa awapa somo Waislamu Kasulu.

   Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Msikiti mkuu  Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wilaya Kasulu mjini Sheikh Mzee Motawa amesema  waumini wa dini ya Kiislamu wanapaswa kuwa na tabia njema ili kumuenzi mtume Muhammad (S.A.W) katika sikukuu ya Maulid.

Akizungumza na Buha FM  Sheikh Mzee  kwa niaba ya Sheikh wa Wilaya, leo September 16, 2024 katika msikiti mkuu wa Kasulu baada ya mkesha wa maulidi na kusema kuwa tabia njema ndio msingi aliyoacha mtume Muhammad (S.A.W) kwa waumini wa dini hiyo.  

"Mhimu sisi tunatakiwa kufuata mwenendo na tabia za mtume Muhammad  (S.A.W) kwa sababu mwenyezi Mungu anasifia Mtume kuwa tabia bora na nikiigizo chema kwetu" Amesema Sheikh Mzee.

Aidha Sheikh Mzee ameongeza kwa kuwaasha waumini wa dini ya kiislamu kutunza na kuendeleza amani ya nchi kwani ni moja ya mafundisho aliyoyafundisha mtume Muhammad (S.A.W). 

"Amani ni moja kati ya mafundisho mhimu aliyotuachia Mtume kutunza na kuiendeleza amani tuliyonayo kwa sababu moja ya tunu ya taifa letu ni amani kwa sababu mtume alitumia njia ya amani kusambaza dini ya Uislamu" Amesema Sheikh Mzee. 

Kwa upande wa waumini wa dini ya kiislamu wamesema kuwa wanasheherekea sikukuu ya Maulid kwa kufuata kile alichofundisha Muhammad (S.A.W) kabla ya kifo chake.

 Waumini wa dini ya kiislamu husheherekea sikukuu ya Maulid ikiwa ni kuzaliwa kwa  Muhammad (S.A.W) katika tarehe 12 ya mwezi wa Rabi al-Awwal katika mwezi wa tatu kwa kalenda ya kiislamu. 

Mwandishi; Ramadhani Zaidy.

Post a Comment

0 Comments