Shinyanga yaadhimisha siku ya usafi Duniani.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote ndani ya Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa masoko na magulio yote yanafanyiwa usafi kwa kuwa ndio maeneo makubwa yenye mkusanyiko wa watu wengi zaidi.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 20 Septemba, 2024 wakati alipoongoza wananchi wa Mkoa huo kusafisha mazingira katika soko la Nguzonane lililopo Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Usafisafi Duniani ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika Manispaa ya Shinyanga.

"Nitumie nafasi hii kuwaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote ndani yaMkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa masoko na magulio yote katika maeneo yanu yanafanyiwa usafi na kuwa safi wakati wote ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kwakuwa ndiyo maeneo ambayo chakula kinapatikana na ndipo kwenye mkusanyiko wa watu wengi zaidi"Amesema RC Macha.

Tanzania maadhimisho haya yameanza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na kuanziahapo kila ifikapo tarehe 20 Septemba  huwa ni maadhimisho yake ambapo kauli mbiu ya maadhimisho ya mwa huu inasema "Uhai Hauna Mbadala, Zingatia Usafi wa Mazingira Siku ya usafishaji Duniani"(WORLD CLENAUP DAY)

Katika historia inataja kuwa nchi ya Estonia huko ulaya Kaskazini ambapo asilimia 4 ya watu walijitokeza pasipo shuruti ya serikali kufanya usafi wamazingira nchi nzima kwa masaa kadhaa tu, jambo hili lileta muamko na mvuto wakipekee kwa jamii nzima na serikali,likapata kibali wakati huo liliongozwa na kauli mbiu “NCHI MOJA, SIKU MOJA”. hivyo nakuifanya nchi hiyo kutambulika kama mwanzilishi wa siku hiyo

Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga manamo tarehe 10 Agosti, 2023 ilitangazwa na kupongezwa  na Baraza la Madiwani kwa ushindi wa usafi na utunzaji wa mazingira iliyoshindanishwa na Halmashauri nyengine 5 katika Mkoa wa Shinyanga.

Mwandishi; Ellukagha Kyusa

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments