Simba na Yanga zatinga kibabe hatua ya makundi 'CAF'.

Timu ya Simba imeendeleza historia ya kulinda heshima ya uwanja wa nyumbani na kutinga hatua ya makundi katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika CAF baada ya kuishushia kipigo cha magoli 3-1 Al Ahly Tripol ya Libya katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam Septemba 22.2024.

Wekundu wa Msimbazi wanaingia hatua hiyo ya makundi kwa jumla ya magoli “aggregate” ya 3 kwa 1 na kufanya Simba kuandikisha historia nyingine Afrika ya kutinga hatua ya makundi mara sita mfululizo ikiwa ni mara nne kwa Klab Bingwa Afrika na mara Mbili kwenye kombe la Shirikisho huku Simba ikifuzu mara nyingi zaidi katika hatua ya makundi kutokaTanzania.

Licha ya matokeo hayo mashabiki walitahamaki baada ya mwamzi mshika kibendela kukataa goli lililofungwa katika kipindi cha pili na Lionel Ateba na kusadikika kuwa ni mpira wa kuotea mashambiki wengi walighazabika na kumtupia lawama mwamzi huyo.

Kwa upande wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika timu ya Yanga Sc ilitinga hatua ya makundi kwa ushindi wa kishindo baada ya kuidhibu CBE ya nchini Ethiopia magoli 6-0 na kuifanya timu ya Wananchi kuweka historia ya kutinga hatua ya makundi mara mbili mfululizo.

Wananchi Yanga Sc wanatinga hatua ya makundi kwa kuishushia kipigo kizito CBE kwa jumla ya magoli 7-0 ikiwa ni matokeo mazuri na yakuendeleza ubabe wa Yanga baada ya msimu uliopita kukiwasha hadi hatua ya robo fainali mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba Sc na Yanga Sc wanasubiri kuona watapangwa kundi lipi na wapinzani gani katika hatua ya kuwania kufuzu hatua ya makundi na kukata tiketi ya robo fainali huku wakijihakikishia kujikusanyia alama za ubora wa klabu shiriki za timu Afrika.

Mwandishi; Eunice Jacob

Mhariri; Sharifat Elias


Post a Comment

0 Comments