Simba Sc, Yanga Sc tayari kwa michuano Afrika (CAF).

Timu ya Simba SC wamesafiri kuwafuata Al haly Tripol ya Libya kucheza michuano ya Kombe la shirikisho  Barani Afrika katika ya mzunguko wa pili kusaka kufuzu hatua ya makundi utakaopigwa jumapili septemba 15,2024 majira ya saa mbili usiku kwa masaa ya  Afrika mashiriki.

Kikosi cha Simba kimehusisha wachezaji 22 kuelekea Libya huku wachezaji wa 4 waliokuwa kwenye majuku ya timu za Taifa wakitarajiwa kusafiri  kupitia Misiri hadi Libya baada ya kumaliza majukumu ya kitaifa huku wakitarajiwa kufika siku moja na wachezaji wengine waliopitia Uturuki.

Simba Sc wanahitaji mchezo huu zaidi kuendeleza mafanikio walio yapata miachano mbalimbali Afrika na kufuta kasumba ya kuisfhia hatua ya robo fainali.

Katika hatua nyingine kikosi cha wananchi, Yanga Sckimewasili Nchini Ethiopia tayari kuvaana na CBE mchezo wa mzunguko wa pili wa kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Barani Afrika utakao pigwa Septemba 14,2024  mjini Addis Ababa.

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema amesafiri na baadhi ya wachezaji ambao hawakuitwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa kwenye michuano ya kuwania kufuzu AFCON, 2025 nchini Morocco huku akibainisha  wachezaji 14 waliokosekana kwenye safari wataungana na timu nchini Ethiopia kupambania timu yao katika mchezo huo.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga na Bemchi la ufundi la timu hiyo wakiwa wakiwa Tayari kwa Safari kuelekea Nchini Ethiopia kwa ajiri ya mchezo dhidi ya CBE  ya Ethiopia.(Picha :Yanga SC)

Yanga wanatakiwa kushinda mchezo huo muhimu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua za makundi ya Klabu bingwa Barani Afrika.

Hata hivyo Timu mbili kutoka Tanzania Simba na Yanga ndizo zinawakilisha katika hatua ya mashindano makubwa barani Afrika ikiwa Yanga wanashiriki katika ligi ya Mabingwa  huku simba wakishiriki  michuano ya Shirikisho barani Afrika.

Mwandishi; Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments