Simba Watoshana Nguvu na Al Ahali Tripol.

Baada ya matokeo ya timu Simba SC kwenye uwanjawa ugenini nchini Libya dhidi ya Al Ahali Tripol ulio tamatika kwa sare tasa ya bila kufungana, kocha wa timu ya hiyo Fadlu Davis amesema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo na kuwa pongeza wachezaji kujitoa licha ya  presha kutoka kwa  mashabiki timu Al Ahali Tripoli.

Mchezo huo ulichezwa majira ya saa 2 usiku katika dimba la Juni 11 mjini Tripoli na kutamatika kwa sare hiyo,kocha Davis amesema safu yake ya ulinzi imefanya kazi kubwa na kuahidi mapungufu yaliyojitokeza watayafanyia mrekebisho katika mchezo wa marejeano Septemba 20,2024 katika Uwanja  wa Benjamini Mkapa Jijini Dar Es Salaam. 

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu ya Simba SC Ahmed Ally ametoa taarifa kuwa timu hiyo inatarajiwa kutoka Libya kwenda Uturuki siku ya jumanne na kufika nchini Tanzania siku ya jumatano alfajiri tayari kwa mazoezi ya maandalizi ya mchezo ujao huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kushangilia timu yao.

"Tunawahitaji mashabiki na wapenzi wa soka kote nchini kuja uwanjani iwe full house kuwapa hamasa zaidi wapambanaji wetu na tunaamini kwa mbinu za mwalimu Davis tutapata matokeo yenye kutupa nafasi ya kufuzu hatua ya makundi katika michuano hii ya kombe la Shirikisho Afrika CAF"

Kwa upande wa Mchazaji wa timu ya Simba SC Shomar Kapombe amesema mechi ilikuwa ngumu hivyo wanajipangha kwa mechi ya marudiano ili waweze kufanya vizuri na kupata matokeo ya kuwapeleka hatua inayofuata.

"Hakuna kinacho shindikana tutarudi kwenye uwanja wa mazoezi na kufajinoa zaidi hasa safu ya ushambuliaji ili kupata magoli mengi natuweze kuvuka hatua tuliopo sasa" Amesema Kapombe.

Ifahamike Timu ya Simba ina historia nzuri ya kupata matokeo katika uwanja wa Benjamini Mkapa katika michuano ya kimataifa huku wapinzani wao wakiwa na historia mbaya katika aridhi ya Tanzania, ikiwa Oktoba 15, 2021 walipoteza mabao mawili 2-0 dhidi ya Biashara United ya Mara kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

Mwandishi; Eunice Jacob

Post a Comment

0 Comments