Simba yajipanga kikamilifu kuwavaa Al ahli


Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally amesema kuwa timu ya Simba inaendelea kujipanga kikamilifu kuelekea mchezo wa marudiano na timu ya Al-Ahli Tripoli kutokea nchini Libya katika kombe la shirikisho barani afrika.

Amesema hayo septemba 18,2024 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusema kuwa maandalizi ya kuelekea mchezo huo ni ya kiutofauti kulingana na mpinzani wanaye kwenda kukutana naye septemba 22,2024.

“maandalizi ni makubwa kuelekea mechi yetu (Simba SC) na Al-Ahli kwa sababu mchezo huu ni wa kiutofauti kulingana na mpinzani wetu lakini pia mchezo huu ni wa hatua ya mtoano na bado haujaisha uko 50 kwa 50 lazima tujiandae ipasavyo” amesema Ahmed Ally

Ahmed ally  amewaomba na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuwapa hamasa wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo kuelekea mchezo huo.

“Kila mwanasimba tunapaswa kusimama na timu yetu bila kujali ukumbwa wa mashindano niwaombe na niwatake wanasimba siku ya jumapili twendeni tukajaze uwanja ili tuipe ushindi simba yetu na tuingie makundi” amesema Ahmed Ally

Mchezo wa awali ulichezwa katika uwanja wa Tripoli international stadium mjini Tripoli uliopo nchini Libya ambao ulitamatika kwa suluhu ya bila kufungana ambapo mchezo wa marudiano utashuhudiwa  katika uwanja wa Benjamin Mkapa septemba 22,2024.

Mwandishi; Ramadhani Zaidy.

mhariri;Ellukagha Kyusa


Post a Comment

0 Comments