Taifa Stars kusaka alama 3 dhidi Guinea.

    Picha:TFF

Mashindano yanayoendelea kwa Timu za mataifa ya Afrika kusaka Tiketi ya kufuzu Afcon timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars iliyopo kundi H wameendelea kujinoa kuelekea mchezo wao wa pili septemba 10,2024 nchin Ivory Coast dhidi ya Guinea.

Kaimu kocha mkuu wa Taifa stars Hemed Suleiman amezungumzia maandalizi kuelekea mchezo wao wa kufuzu Afcon 2025 nakusema kuwa wachezaji wake wapo vizuri hakuna majeruhi hivyo wapo tayari kupata matokeo mazuri.

“Niwaombe wadau na wapenzi wa soka kuacha kulaumu badala yake watoe ushirikiano ili kulisapoti Taifa kuinuka kimchezo sababu wachezaji wengi ni wageni na vijana wadogo”

Mchezaji wa Taifa Stars na Göztepe S.K ya Uturuki ,Novatus  Miroshi Dismass amezungumza baada ya mazoezi na kusema wapo tayari kurekebisha makosa ya mchezo uliopita na kuvuna alama tatu mbele ya wapinzani wao Guinea.

“Tumejiandaa kupata matokeo mazuri yatakayo fanya tusonge mbele kwanza hakuna mchezaji mwenye hofu juu ya mchezo huo maana tumejinoa vya kutosha”

Taifa Stars inakwenda kwenye mchezo huo wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kudondosha alama mbili[2] na kufanikiwa kugawana alama moja [1] baada ya dakika tisini kutamatika kwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Ethiopia katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar Es Salaam Septemba 4, 2024.

Mwandishi; Eunice Jacob


Post a Comment

0 Comments