Mchezo huo umechezwa majira ya saa 1 jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki huku Tanzania akipata mabao hayo mawili baada ya kutanguliwa na wapinzani wao kupata goli la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wa timu ya Guinea, Mohamed Bayo mnamo dakika 57 baadaya kipindi cha kwanza kutamatika bila kufungana.
Feisal Salum kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars na Azam FC ya Dar es salam aliweka goli la kuswazisha mnamo dakika ya 61 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Wazir Junia na kupiga Shoti kali lililozama kimyani na matokeo kusoma 1-1.
Timu ya Tanzania, Taifa Stars ilionyesha juhudi za kushambulia na kulinda isiruhusu mashambulizi katika goli lake na mbinu za mwali kwa kufanya mabadiliko kadhaa yaliweza kuwanyima uhuru wapinzani kulifikia lango la Taifa Stars baada ya kumuingiza Himid Mao Mkami na kutuliza Dimba la kati
Taifa Stars iliweza kupata bao la kuongoza mnamo dakika ya 88 kupitia kwa kiungo Mkabaji wa Yanga Afrika ya Dar es Salaam Mudathir Yahaya kwa kumalizia mpira uliopigwa na kiungo mshambuliaji Feisal na kumshinda mlinda mlango wa Timu ya Guinea Ibrahim Kone na kuifanya Stars kuibuka na ushindi huo.
Tanzania, Taifa Stars imefikisha alama4 ikiwa nafasi ya pili katika kundi H huku Congo DR wakiwa nafasi ya kwanza wakiwa na alama 6 baada ya kushinda mnichezo yao yote miwili kati ya Guinea na Ethiopia, Taifa Stars imebakiza michezo miwili ya nyumbani kati ya Congo na Guinea kwa ajili ya marudio huku michezo ya nje ni kati ya Ethiopia na Congo ambao wataanzia nyumbani na kumalizia ugenini.
Mwandishi; Sharifat Shinji
0 Comments