Tamko migogoro ya wakulima na wafugaji.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewaasa wafugaji wa jamii ya Wasukuma wanaoishi katika kata ya Ndalila Wilayani Songea, kuhakikisha kuwa wanaishi kwa amani na wakulima wa jamii zingine waliopo wilayani humo.

Bashe amesema hayo katika Kata ya Njalila, Wilaya ya Songea wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya kilimo kwenye mikoa mbalimbali nchini ambapo amezungumza na wananchi kuhusu kero zao na mipango ya serikali katika kutatua kero hizo.

Aidha amewaeleza viongozi wa taasisi za serikali kuchukua hatua na kufanya usanifu wa barabara na bwawa kwa ajili ya kumwagilia hekari 6000, pamoja na kujenga zahanati na kituo cha afya.

"Mkurugenzi wa Umwagiliaji na mhandisi wa Umwagiliaji mkoa pia yupo hapa, Kwa mwaka huu tutaanza na usanifu ambapo wataalamu watakuja kwa ajili ya kujua gharama, na masuala mengine muhimu kabla ya Kuanza utekelezaji"Amesema Bashe.

Waziri Bashe amebainisha mpango wa wizara kununua mazao kutoka kwa wakulima, kwa lengo la kuwaepusha wakulima kupata hasara za kuuza mazao yao kwa bei ya chini.

"Mwenyekiti wa Skimu kasema mnauza mpunga kwa elfu sitini kwa gunia, serikali itauangalia mpunga mliovuna na tutanunua gunia moja la kg 90 kwa shilingi 81,000 na serikali itaununua wote"

Kupitia ziara hiyo, migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa ikisumbua maeneo mengi nchini kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kibinadamu huku maeneo yanayotajwa kuwa na migogoro hiyo ni Songwe,Rwukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na mkoa wa Kigoma.

Mwandishi; Ellukagha Kyusa

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments